- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na, Shani S.Amanzi
Naibu Katibu Mkuu Taifa UWT Mhe.Jesca Mbogo ( picha; wa tatu kutoka kulia ) awataka wanawake wa Chemba wasiishi kwa majungu badala yake washirikiane kwa pamoja kwani Serikali ya awamu ya tano ni hapa kazi tu wanapaswa kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.
“kumekuwa na zana ya ujasiriamali ulioanza toka zamani lakini kutokana na dunia kukua kiuchumi, sayansi na teknolojia ni vyema nanyi kuwa wabunifu katika kukuza ujasiriamali wenu. Lengo la kuja leo kwenu ni kuwapa hamasa ili muweze kujikwamua kiuchumi katika makundi ya akina mama na walemavu wa jinsia zote kwa sababu Chama cha Mapinduzi kinawajali na kuwathamini wananchi wote kwa kuwaletea maendeleo ya nchi nzima”aliongeza kwa kusema Mhe.Jesca Mbogo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga alisema “katika wilaya ya Chemba tunaendelea kuweka kipaumbele kwa wananchi hususani katika mambo yatakayo wasaidia kimaendeleo kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya na Halmashauri. Pia Wilaya imeweka mkakati wa kutengeneza barabara zake, kubuni njia mbalimbali za kupata mapato ya ndani na kutatua kero ya maji kwa wananchi”.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba amesema Halmashauri ya Wilaya ya Chemba imetoa mikopo kwa kina mama pamoja na vijana kwa asilimia 10.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 20/9/2019 kwa kufanya mkutano wa hadhara na wajasiria mali pamoja na walemavu.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.