- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndugu Hassan Mnyikah amewataka Maafisa Elim Kata, na Walimu wakuu wa shule za awali na msingi Wilayani Chemba kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Mnyikah ameyasema hayo tarehe 29, Julai 2025 wakati akifungua mafunzo ya uongozi wa ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Halmashauri yaliyofanyika katika ukumbi wa VETA Wilayani Chemba.
"Ualimu ni wito, tumieni mafunzo haya kama fursa ili mtoke na mbinu mbalimbali za kuwawezesha wanafunzi wetu kufanya vizuri Zaidi katika mitihani yao na hili ndilo lengo letu" amesema Mnyikah
Sambamba na hilo Mnyikah pia amewaomba Viongozi hao wa elimu kufanya mabadiliko katika sekta hiyo muhimu kwa lengo la kuboresha viwango vya ufaulu na kuongeza kuwa yeye ni msikivu na yuko tayari kushauriana na kushirikiana nao.
Mapema akizungumza na Viongozi hao wa elimu ngazi ya Halmashauri Mratibu wa Program ya Shule Bora Bi Amina Rajab amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji Maafisa elimu Kata na Walimu Wakuu lengo likiwa ni kujipanga kikamilifu ili kuhakikiksha Wanafunzi wanafanya vuzuri katika masomo yao.
Aidha, Bi Amina Rajab amesema kuwa Maafisa elimu Kata, na Walimu Wakuu wanao wajibu wa kujitathmini na kutafuta mbinu bora za kufanya ili kuongeza kiwango vya ufaulu kwa Wanafunzi wa elimu ya awali na msingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha manunuzi Ndugu Salvin Musa amesema kuwa Maafisa elimu Kata na Walimu Wakuu ndio wasimamizi Wakuu wa miradi ya Serikali inayotekelezwa katika maeneo yao hivyo amewaomba washirikiane kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora na kwa wakati na wawahamasishe Wananchi kushiriki katika utekekezaji wa miradi hiyo ili kupunguza gharama.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.