- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndugu Hassan Mnyikah tarehe 30, Julai 2025 ameongoza kikao cha Kamati ya lishe robo ya nne Aprili - Juni 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Mnyikah ameelekeza Wajumbe wa kamati ya lishe kuendelea kuwahamasisha Wazazi/ Walezi kuchangia chakula cha Watoto wao Shuleni.
"Siyo jambo jepesi kwa mwanafunzi kufanya vizuri darasani huku akishinda njaa kuanzia asubuhi mpaka jioni, wahamasisheni Wazazi wachangie chakula shuleni na ikibidi sheria ndogondogo zitumike kuwawajibisha" amesema Mnyikah
Akiwasilisha Tarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika kipindi cha robo ya nne Aprili - Juni 2024/2025 Afisa lishe wa Wilaya Bi Faith Temu ametaja mafanikio yaliyopatikana katika robo hii ya nne ikiwa ni pamoja na ufanyikaji wa vikao vya lishe, usimamizi shirikishi na ukaguzi wa usalama na ubora wa chakula umefanyika kwa 100%, Vijiji vyote 114 vimefanya SALIKI kwa kufuata mwongozo, Asilimia ya Wanafunzi wanaopata chakula shuleni imeongezeka ukilinganisha na robo iliyopita.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.