- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC OKASH AWATAKA WATENDAJI KUHAMASISHA UTOAJI WA CHAKULA SHULENI
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji Wilayani Chemba kuhamasisha Waananchi/ Wazazi juu ya utoaji wa chakula shuleni.
DC Okash ameyasema hayo mapema tarehe 29, Julai 2025 wakati akiongoza kikao cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha Aprili - Juni 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
DC Okash amesema kuwa lishe ni ajenda ya Kitaifa hivyo amewataka Watendaji kuitisha mikutano na Wananchi/ Wazazi na kuwahamasisha juu ya utoaji wa chakula shuleni na pia amewataka Watendaji hao kuwasiliana na Walimu wa shule ili kujua mahitaji halisi ya chakula kwa kila Shule.
"Mpaka kufika mwishoni mwa mwezi Agosti tuwe tumepata chakula cha kutosha kwaajili ya Wanafunzi Shuleni" amesema DC Okash
Aidha, Mkuu Huyo wa Wilaya ya Chemba amewaelekeza Maafisa lishe wa Wilaya kuwawezesha Watendaji ili waweze kutekekeza majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanaofanya vizuri ili waendelee kufanya vizuri zaidi katika maeneo yao.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.