- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi wa darasa la saba Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wameahidi kufanya vizuri katika mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi kwa asilimia 100%.
Ahadi hiyo imetolewa katika hafla ya chakula cha pamoja iliyoambatana na maombi maalum pamoja na nasaha kutoka kwa Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi, Wazazi, Wazee maarufu, Viongozi wa Serikali ya Kijiji na Kata, na Viongozi wa Dini.
Hafla hiyo ya chakula cha pamoja imeongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bi Juster Katemana katika Shule ya Msingi Kidoka, Shule ya Msingi Kwamtoro hafla hiyo imeongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya Bi Salah Ngalingasi, Shule ya Msingi Churuku hafla hiyo imeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndugu Hassan Mnyikah, na Shule ya Msingi Goima ameongoza AfisaTarafa wa Tarafa ya Goima Bi Joyce Olotu.
Akiongea katika Shule ya Msingi Kidoka ambapo alikua Mgeni Rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bi Juster Katemana amesema Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilitenga siku ya tarehe 4, Septemba 2025 kuwa ni siku ya Wazazi, Walimu,Wanafunzi, Kamati za Shule, Wazee maarufu , Viongozi wa Kata na Vijiji, na Viongozi wa Dini kupata chakula cha pamoja kuwaombea na kuwatia moyo Wanafunzi wa darasa la saba ambao wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa tarehe 10 -11, Septemba 2025.
Bi. Juster Katemana amewasihi Wanafunzi hao kujisomea kwa bidi katika siku hizi chache zilizobakia ambapo pia amewasisitiza Wanafunzi hao kuendelea kumuomba Mungu kila mmoja kwa Imani yake ili waweze kufanya vizuri Zaidi.
Mwakilishi huyo wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya amemshukuru Afisa Elimu Msingi Ndugu Josephat Ambilikile kwa maandalizi ya tukio hilo muhimu.
Aidha, Bi Juster Katemana amewashukuru Wazazi kwa ushirikiano waliounyesha pamoja na kuchangia chakula cha Wanafunzi hao ambacho kimewawezesha Wanafunzi hao kuendelea na masomo yao wakiwa na afya njema.
Mwakilishi huyo wa Mkuu wa Wilaya akatumia fursa hiyo kuwaomba Wazazi kutowakatisha Watoto tamaa pale watakapofaulu kwenda Sekondari na kuongeza kuwa Watoto wote watakaofaulu waende Shule hata kama watakua hawajapata sare za shule.
Akizungumza kwa niaba ya Wanfunzi wenzake Mwanafunzi Sabrati Abasi amewashukuru Wazazi, Walimu, Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi, Viongozi wa dini, Viongozi wa Serikali ya Kijiji na Kata kwa kujumuika nao katika chakula cha pamoja, na kuwaombea ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
“Nakuhakikishia Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuwa Wanafunzi wote wa darasa la saba katika shule ya msingi Kidoka tutafaulu kwa sababu Walimu wetu wametuandaa vizuri, na tumefanya mitihani ya kutosha “ amesema Sabrati Abasi.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.