- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndugu Hassan Mnyikah tarehe 8, Septemba 2025 ameongoza timu ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kukagua miradi ya maendeleo sekta ya afya na elimu robo ya nne Aprili – Juni 2024/2025.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ukamilishaji wa zahanati ya Takwa, Ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Ovada, ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Lalta, ujenzi wa mradi wa miundombinu ya usafi wa mazingira kituo cha afya Kwamtoro, ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Mondo, ujenzi wa kituo cha afya Dalai, ujenzi wa chumba cha darasa shule ya msingi Hamai, ukamilishaji wa ujenzi zahanati ya Songolo, ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati ya Madaha, pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi Mchiga.
Akizungumza katika mradi wa zahanati ya Takwa Mkurugenzi Mnyikah ameitaka Kamati ya ujenzi pamoja na Viongozi wa Kata na Vijiji kuendelea kuwaelimisha Wakazi wa enea hilo kuchangia nguvu kazi zao ili ujenzi wa mradi huo uweze kukamilika.
“Tunatoa nafasi ya mwisho kwa Kijiji hiki kuchangia nguvu kazi ili ujenzi wa mradi huu uweze kukamilika, vinginevyo fedha ambazo zipo benki shilingi milioni 60 tutazihamshia sehemu nyingine ambako wana uhitaji na utayari wa kuchangia nguvu kazi zao ili waweze kupata huduma kama hii” amesema Mkurugenzi Mnyikah
Sambamba na hilo Mnyikah ameitaka Kamati ya ujenzi pamoja na Viongozi
wa Kata na Vijiji Kata ya Kinyamsindo kutokutumia njia moja tu ya kuchangia nguvu kazi bali endapo baadhi ya Wakazi wa eneo hilo wametingwa na majukumu na kupelekea kukosa muda wa kwenda kuchangia nguvu kazi basi Wakazi hao wachangie fedha ambazo zitatumika kunnuna mahitaji muhimu ya ujenzi wa mradi huo.
Aidha, Mkurugenzi Mnyika ameielekeza Kamati ya ujenzi pamoja na Viongozi wa Kata na Vijiji Kata ya Kinyamsindo kutoa taarifa ya maendeleo ya ya utekelezaji wa mradi huo hususan uchangiaji wa nguvu kazi za Wananchi mapema tarehe 10, Septemba 2025.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mnyika amezipongeza kamati za ujenzi pamoja na Viongozi wa Kata na Vijiji katika mradi wa kituo cha afya Ovada, ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Lalta, ujenzi wa mradi wa miundombinu ya usafi wa mazingira kituo cha afya Kwamtoro kwa uchangiaji wa nguvu za Wananchi, na utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzingatia ubora .
Hata hivyo , katika miradi yote aliyoitembelea kwa kushirikiana na timu ya Wataalam, Mnyika amehimiza utunzaji wa vifaa, uwekaji wa kumbukumbu za mapokezi ya vifaa pamoja na utunzaji wa nyaraka za manunuzi.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.