- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash tarehe 11, Septemba 2025 ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndugu Benjamini Gerome Mlesa aliyekuwa akihudumu nafasi ya Afisa Biashara.
Kwa upande wa Ofisi ya Mkurugenzi, Ndugu Hassan Mnyikah ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba aliambatana na Mkuu wa Idara ya Utumishi Ndugu Hillary Mniachi pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kutoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao.
Ikumbukwe Ndugu Benjamini Gerome Mlesa alifariki tarehe 09/09/2025 katika Hospitali ya DCMC Ntyuka Jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba itamkumbuka daima kwa uchapakazi wake katika kulijenga Taifa.
Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa Amani. Amina
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.