- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kauli hiyo imetolewa na Washiriki wa SHIMISEMITA 2025 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Utumishi Ndugu Hillary Mniachi mapema tarehe 03, Septemba 2025 wakati wakikabidhi kombe na medal za ushindi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba Ndugu Hassan Mnyikah.
Akizungumza na Washiriki hao Mara baada ya kukabidhiwa kombe na medal Ndugu Mnyikah amewapongeza washiriki hao kwa kufanya vizuri licha ya changamoyo kadhaa walizokutana nazo wakati wa mashindano hayo.
“Mmetuheshimisha Wanachemba, nimefurahi sana, na kwa ushindi huu nawaahidi kuwa mwakani tutajipanga vizuri ili mfanye vizuri zaidi “ amesema Mnyikah
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utumishi Ndugu Hillary Mniachi amesema kuwa katika mashindano ya SHIMISEMITA 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba iliibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa uchoraji, mshindi wa kwanza kwa mbio za mita 100, mshindi wa pili mbio za mita 400, na mshindi wa kwanza mbio za mita 100 x 4 relay
Aidha, Ndugu Mniachi amemuomba Mkurugenzi Mnyikah kuwatazama kwa jicho la kipekee Washiriki hao wa SHIMISEMITA 2025 kutokana na bidii na uvumilivu waliouonyesha katika mashindano hayo.
Akizungumza kwa niaba ya Washiriki wenzake Ndugu Jonson Limbe amemshukuru Mkurugenzi Mnyikah kwa kuwatia moyo na kuwawezesha kushiriki mashindano hayo ambapo pia ameahidi kuwa mwakani watafanya vizuri zaidi katika mashindano hayo kwani wanatarajia kuanza mapema maandalizi ya kujinoa kwenye michezo mbalimbali.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.