- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Afisa Mazingira Ndg. Mohamed Semdoe amesema zoezi la upandaji miti katika wilaya ya Chemba linaendelea vizuri na tarehe 25/1/2018 jumla ya miche ya miti 12,500 imepokelewa kutoka TASAF Kondoa kwa ushirikiano na TFS.
Ndg. Semdoe amesema zoezi la mapokezi linaendelea na tunatarajia kupokea jumla ya miche ya miti 400,000 ambayo itasambazwa vijijini kwa ajili ya kupandwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu wa kuifanya Dodoma ya kijani.
Awamu ya kwanza jumla ya miche ya miti 3,500 imepandwa mwezi Desemba, 2017 katika vijiji vya kidoka, Kelema, paranga, kambi ya nyasa, Kelema kuu na Makao makuu ya wilaya ya chemba.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.