- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mapema tarehe 27, Septemba 2025 lilifanyika Bonanza la mechezo la mechi za kirafiki baina ya Watumishi wa Umma Chemba DC na Kondoa DC lililobeba ujumbe wa “Shiriki kupiga kura kwa maendeleo ya michezo”
Bonanza hilo la michezo lililofanyika viwanja vya shule ya Msingi Chemba lilihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu ya Kondoa DC iliibuka na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya Chemba DC, michezo mingine ni pamoja na mchezo wa bao na mchezo wa draft.
Akizungumza katika bonanza hilo la michezo Afisa michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Gerishom Mbehong’hali alisema kuwa Watumishi wa Chemba DC wamefurahi kushiriki michezo mbalimbali pamoja na Watumishi wa Kondoa DC ambapo pia alitoa shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndugu Hassan Mnyikah kwa kuwezesha Wanamichezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kushiriki kikamilifu Bonanza hilo.
“Tumecheza na kufurahi pamoja , tumeimarisha afya na kubadilishana ujuzi, Nawashukuru sana Kondoa DC kwa kuendeleza mshikamano, ushirikiano wa kikazi na kijamii” aliongeza Ndugu Gerishom
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Michezo na Utamaduni Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndugu Mohamedi Chillo Akizungumza kwa niaba ya Wachezaji wa Kondoa DC alisema kuwa ushiriki wao katika bonanza hilo umetokana na uwezeshwaji mzuri kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndugu Shaaban Millao.
Bonanza hilo la michezo liliandaliwa kwa ushirikiano wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kupitia Vitengo vya Michezo na utamaduni na kufanyika ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.