- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Timu ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tarehe 15, Oktoba 2025 imefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo sekta ya Afya na Elimu robo ya kwanza Julai – Septemba 2025/2026
Ujenzi wa wa Kituo shikizi cha thawekwa kilichopo Kijiji cha Porobanguma Kata ya Kwamtoro ni miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ambapo kituo hiki kinahusisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na Ofisi kwa jumla ya fedha kiasi cha shlingi milioni 27,200,000, milioni 25,000,000 kutoka Serikali Kuu na milioni 2,200,000 kutoka mfuko wa Jimbo.
Kituo hiko shikizi cha Thawekwa kwasasa kimefikia hatua ya kuezekwa na kina jumla ya Wanafunzi 300 wa darasa la awali hadi darasa la tatu na Walimu 3 tu.
kufuatia hali ya kusuasua kwa ujenzi wa kituo hiko kutokana na nguvu kazi hafifu kutoka kwa Wakazi wa eneo hilo Timu ya Wataalam kutoka halmashauri imewataka viongozi wa Kijiji cha Porobanguma kuendelea kuhamasisha Wakazi wa Kijiji hiko na kuhakikisha ujenzi wa kituo hiko unakamilika kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Katika hatua nyingine Timu hiyo ya Wataalam imeitaka Kamati ya ujenzi wa Kituo cha Walimu (Teachers Resources Centre)kuwashirikisha Wananchi wa eneo hilo ili waweze kuchangia nguvu kazi pamoja kufanya kazi kwa ukaribu na Kitengo cha manunuzi pamoja na maeneo mengine ndani ya Halmashauri ambayo yametekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili waweze kupata uzoefu na kushirikiana katika kutatua changamoto zinazowakwamisha katika utekelezaji wa mradi huo.
Ujenzi wa kituo cha Walimu ambao upo katika hatua za walia za ujenzi (Teachers Resources Centre)kinachojengwa Kata ya Farkwa unahusisha ujenzi wa vyumba viwili na matundu mawili ya vyoo kwa fedha kiasi cha shilingi milioni 46,000,000 kutoka Serikali Kuu.
Aidha, Timu hiyo ya Wataalam imeipongeza Serikali kwa uboreshaji wa Jengo la Wazazi na watoto wachanga hususan Watoto wanaozaliwa kabla ya umri( Njiti) katika Hospitali ya Wilaya lililofanyiwa maboresho kwa fedha kiasi cha shilingi milioni 25,000,000 fedha kutoka Serikali Kuu ili kuimarisha na kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa Wazazi na Watoto wachanga.
Hata hivyo, Timu hiyo ya Wataalam ilikamilisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi katika ujenzi wa Shule mpya ya mkondo mmoja na nyumba ya Walimu 2 in 1 unaofanyika eneo la Chemba mjini kwa fedha kiasi cha shilingi milioni 397,200,000 (BOOST)
Ujenzi wa mradi huuu ambao uko katika hatua za awali unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu ili shule hiyo ipokee wanafunzi wapya wa madarasa ya awali na msingi ikiwa ni pamoja na kupunguza mlundikano wa Wanafunzi katika shule ya msingi Chemba mwaka ujao 2026.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.