- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipotembelea ujenzi wa mradi wa Kituo cha afya Dalai ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi kutembelea miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Chemba Oktoba 2, 2025 ambapo ametembelea miradi ya Elimu na AFya Kata ya Mondo, Dalai na Songolo.
“Ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya huduma za afya katika Wilaya za Mkoa wa Dodoma utasaidia kusogeza karibu na Wananchi huduma bora za afya pamoja na kuokoa maisha ya Wananchi pindi inapotokea dharura ya ajali na matukio mengine yanayohitaji huduma za haraka za kitabibu” amesema RC Senyamule.
Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Dalai unajengwa kwa fedha shilingi milioni 686.5 ambapo fedha kutoka Serikali Kuu ni shilingi milioni 678.7 na michango ya nguvu za Wananchi ni shilingi milioni 10.8.
Akiwa kwenye mradi wa Zahanati katika Kata ya Songolo Mhe. Senyamule amepongeza hatua ulipofikia mradi huo ambapo taarifa ya utekelezaji wa mradi huo imeeleza kuwa mradi huo umegharimu shilingi milioni 60 fedha kutoka Serikali Kuu na nguvu za Wananchi shilingi milioni 10 ili kuunga mkono juhudi za Serikali, mradi huo unatarajiwa kukamilika Novemba 30, 2025 ambapo kwasasa umefikia 65% ya utekelezaji.
Aidha akiwa katika Mradi wa miundombinu ya elimu Shule ya Msingi Mondo ambao unahusisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa shilingi milioni 46 fedha kutoka Serikali Kuu na ujenzi wa matundu 21 ya vyoo kwa shilingi milioni 49.4 fedha kutoka mpango wa SRWSS Mhe. Senyamule amempongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mondo kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na ujenzi wa matundu 21 ya vyoo ambayo yamejengwa kwa kuzingatia ubora.
Ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya elimu Wilayani Chemba unatarajiwa kuongeza viwango vya ufaulu na kuwapunguzia Wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni, ambapo pia kukamilika kwa miundombinu ya miradi ya Afya kutawapunguzia Wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kwenda Vijiji vya jirani kutafuta huduma za afya.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.