- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga amezindua rasmi zoezi la chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi Mashuleni.
Dkt.Semistatus Mashimba amesema Saratani ya kizazi inaweza kuzuilika kwa njia tofauti ila njia kubwa ni hii ya kuweza kupata chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi na chanjo hii inatolewa kwa mabinti walio katika umri wa miaka 9 hadi 14 .
“Pia njia nyingine ni kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini dalili za awali na kupata matibabu stahiki na endapo itagundulika mapema inaweza kuzuilika ,hivyo ni vizuri kwa wakina mama waliofikia umri wa miaka 30 hadi 50 kufika katika vituo vinavyotoa huduma ya upimaji wa saratani ili kubaini afya zao kwani inaonekana wanawake wengi wanaogundulika wanafika wakiwa wamechelewa”aliongeza kwa kusema hayo Dkt.Semistatus Mashimba.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chemba Dkt.Olden Ngasa ameishukuru Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto pamoja na Wadau mbalimbali kwa kuweza kuwaletea chanjo hizo ,ili kuweza kunusuru wanawake na watoto kutokana na vifo vinavyoweza kuzuilika kwa chanjo.
Dkt.Ngasa amesema “inakadiriwa kuwa duniani kote wastani wa wanawake takribani nusu milioni wanagundulika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka,wengi kati ya waathirka wanatokea katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na natumaini zoezi hili la chanjo litafanyika kikamilifu.”
Saratani ya mlango wa kizazi ni mabadiliko ya ukuaji wa seli usio wa kawaida katika mlango wa kizazi,saratani hii ya mlango wa kizazi ina athari kubwa kwa akina mama duniani kote na zoezi hilo la uzinduzi limefanyika katika Zahanati ya Kelema wilayani Chemba tarehe 25/5/2018
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.