- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF umetangaza kuziondoa jumla ya Kaya 156,586 zilizokuwa zikinufaika na TASAF mara baada ya kuimarika kiuchumi ambapo sasa zinaweza kujitegemea pasipo kupata ruzuku.
Kaya hizo ni miongoni mwa kaya zaidi ya Milioni 1.3 zilizo katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mpango huo kilichozinduliwa Februari 2022,ambapo kuondolewa kwake ni baada ya kufanyika tathimini ya hali za ustawi wa maisha yao katika mamlaka zote 186 za utekelezaji.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga amesema uhitimu wa walengwa walioimarika kiuchumi kupitia uwezeshwaji uliofanywa na mfuko huo.
Mwamanga amesema kuwa kwa sasa kaya hizo zina makazi bora, zinaweza kumudu gharama za matibabu, kusomesha watoto na zina vitega uchumi na biashara za uhakika zinazoongeza pato la familia.
“Kwa mujibu wa taratibu za muundo wa mpango, kaya inaponufaika hatua ya kujikimu na kuimarika kiuchumi kwa kuwa na chanzo au vyanzo vya uhakika wa mapato, inapoteza sifa za kuendelea kupokea ruzuku na inadi iondolewe kwenye mpango,” amesema Bw.Mwamanga
Hata hivyo Mwamanga amesema pamoja na kaya hizo zipo kaya nyingine 16,490 ambazo pia zitatolewa kwenye mpango ifikapo Januari mwaka 2023.
Amesema kuwa Kaya hizo zimetoka katika halmashauri za wilaya ya Bagamoyo,Kibaha,Lindi,Chalinze na katika manispaa za Mtwara,Lindi na kutoka Unguja.
Mwamanga amesema kuwa TASAF itaendelea kutoa elimu kwa walengwa kuhusu taratibu za Mpango kuhamasisha ushiriki wa walengwa katika masuala mbalimbali kuwekeza ili wanapohitimu waweze kujihudumia wao wenyewe.
Aidha ametaja njia zilizotumika kuwatambua na kuwaondoa kwenye mpango kuwa ni kuitisha mikutano ya kijamii,kujaza dodoso la taarifa za hali ya uchumi ya kaya na kufanya uhakiki kwa kutumia mfumo maalum wa kuchakata takwimu kwa njia ya kompyuta.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.