- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Katibu Tawala Wilaya ya Chemba Ndg.Nyakia Ally amewataka wananchi wa kata ya Gwandi kutunza Miti ya asili, kuendelea kutunza mazingira na kuepuka kukata miti ovyo .
Ndg.Nyakia aliyazungumza hayo alipokuwa anamtambulisha Mwekezaji wa Mradi wa Nyuki Ndg.Kinyango Ildephonce (aliyesimama mwenye kofia) katika mkutano wa hadhara kijiji cha Gwandi tarehe 2/2/2018.
“Ndugu Wananchi, uwepo wa mwekezaji huyu katika kijiji chenu na Wilaya ni fursa kwetu kupata huduma za kijamii ikiwemo madawati shuleni, huduma za maji na serikali itapata faida kwa njia ya ulipaji wa kodi.”Alisisitiza Katibu Tawala Wilaya.
Naye Mwekezaji wa Mradi wa Nyuki Ndg.Kinyango Ildephonce amesema Nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa na Misitu mingi, na ameona ni vyema aje Mkoa wa Dodoma katika Wilaya ya Chemba kuwekeza katika Ufugaji wa Nyuki na kwa bahati nzuri amekuta kijiji cha Gwandi kina Kikundi cha Ufugaji wa Nyukia ambacho atakuwa nacho bega kwa bega.
Ndg.Ildephonce amesema “Wajumbe wa Serikali ya kijiji mkumbuke katika kikao cha kwanza tulichofanya niliwaeleza kuwa ninachohitaji ni kuwawezesha ujuzi vijana ili watumie fursa hii vyema katika ufugaji nyuki na ni njia ya kuwapatia ajira pia.”
Aidha Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bi.Flora Shija alisema “Nchi yetu ni ya Viwanda vidogo vidogo na vya kati, umaskini utapunguzwa kuanzia ngazi ya kijiji, kata, na Wilaya yetu kwa kuwapatia vijana ajira kupitia rasilimali tulizonazo.”
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Nyuki Ndg. Ally Mpima alitoa ufafanuzi kwa kusema, Mkoa wa Dodoma umeteua Hifadhi za Misitu ya Asili kwa ajili ya Ufugaji Nyuki katika vijiji vya Jogolo kata ya Ovada-ukubwa hekta 2314, Baaba kata ya Ovada-ukubwa hekta 867, Sanzawa kata ya Sanzawa hekta 912, Mialo kata ya Kwamtoro –ukubwa hekta 500.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.