- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga ametoa agizo kwa waganga wote wa kienyeji mkoani Dodoma kuacha kazi za kupiga ramli chonganishi ambazo zimekuwa zikilazimisha jamii kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) ili wakate viungo vyao kwa ajili ya kupata utajiri ambapo siyo kweli.
Mkuu wa Wilaya aliyazungumza hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alipokuwa akizindua siku ya Maadhmisho ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) 09/06/2018 kimkoa wilayani Chemba ambapo kitaifa yatafanyika 13/6/2018 mkoani Simiyu.
Mhe. Odunga amesema Serikali itaendelea kuweka utaratibu mzuri ili kuhakikisha mafuta ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) yanapatikana katika hospitali zote za wilaya na kutoa elimu kuhusu utunzaji wa ngozi.
Mhe. Odunga aliongeza kwa kusema “ kwa wale watakaoshindwa kuwaandikisha watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, kwani Serikali ya awamu ya Tano imetoa fursa ya elimu bure kwa watoto wote”.
Naye Katibu wa chama cha Watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) Tanzania (TAS) Ndg. Hudson Seme amesema kumekuwepo na utata wa kutokuwepo na Takwimu halisi ya juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) ambapo changamoto inachangiwa na jamii kiujumla kwakuwa na imani potofu inayosababisha kutotoa taarifa za watu wenye ulemavu.
“Aliongeza kwa kusema ni vyema watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) wajiunge kwenye vikundi ili waweze kufanya kazi za ujasirimali kwani serikali ya awamu ya Tano kupitia Idara ya maendeleo ya jamii iendelee kuboresha na kutoa misaada mbalimbali kwa kutoa fedha”.
Kauli mbiu yaWatu wenye Ualbino kwa mwaka huu ni ‘’BADILI FIKRA POTOFU DHIDI YA WATU WENYE UALBINO: UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE AFYA, ELIMU NA AJIRA ZAO’’.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.