- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Stephen Wasira ameeleza faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kanda ya Kati iliyopo Kata ya Chemba katika Halmashauri ya Wilaya Chemba.
Wasira ameeleza kuwa Muungano unachochea na kuimarisha biashara baina ya pande mbili lakini pia unaleta aman kwani wananchi wa pande zote mbili wanauhuru wa Kwenda kuishi katika nchi hizo mbili bila masharti yoyote.
Aidha amewapongeza viongozi waasisi wa Muungano huo ambao ni Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Hayati Abeid Amani Karume kwa kuona mbali na kuziunganizha nchi hizi mbili ambapo matunda yake yanaonekana hadi leo.
Hata hivyo amewasihi wananchi kuendelea kuudumisha na kuuenzi Muungano huo ili kuendeleza maono ya viongozi waasisi na kudumisha amani na kukemea wote wanaobeza Muungano kwani hawana nia njema na maendeleo ya wananchi na nchi hizo mbili.
Hata hivyo Wasira ameongeza amewakumbusha wananchi wote ambao bado hawajajiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura kutumia fursa ya kujiandikisha itakapokuja awamu ya pili mapema mwezi Mei Ili kila mmoja apate haki yake ya kikatiba ya kuchagua kiongozi amtakaye katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya Mrs. Sara John Ngalingasi akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo kwa Makamu Mwenyekiti ametumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya Billion nne na Million Mia Moja (4.1) kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya hiyo.
“Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kanda ya Kati umelenga kupunguza adha ya gharama ya nauli kupangiwa shule za mbali kutafuta elimu lakini pia kutoa wigo mpana wa kila mtu kupata elimu Ili kuwa na kizazi kilichoelimika.
Ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM bara imefanyika wilayani Chemba ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo hufanyika kila tarehe 26 Aprili ya kila mwaka ambapo mwaka huu ni miaka 61 toka kutokea kwake na kauli mbiu ya mwaka huu imesema
“Muungano wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa Shiriki uchaguzi mkuu mwaka 2025”.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.