- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya KataJimbo la Chemba wameanza kupatiwa mafunzo ya uchaguzi ya siku tatu leo tarehe 4, Agosti 2025 ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na kuwawezesha wasimamizi wasaidizi kutekekeza majukumu yao ipasavyo.
Mafunzo hayo yanayofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri yamefunguliwa na Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Chemba Ndugu Dominick Ruhamuya ambaye amewataka Wasimamizi wasaidizi kutambua kuwa dhamana waliyopewa kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ni kubwa, nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu, hivyo wanategemewa kuzingatia utendaji wao, wawajibike ipasavyo katika kipindi chote hadi hapo jukumu hili la uchaguzi litakapokamilika.
Aidha, Ndugu Dominick amewaasa Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yao wanao katika uendeshaji wa uchaguzi wasiache kusoma katiba, sheria, kanuni, taratibu, miongozo na wafuate na kutekeleza maelekezo mbalimbali yatakayokuwa yanatolewa na Tume.
"Fanyeni utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo husika na kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani" amesema Ruhamuya
Mafunzo hayo yanajumuisha Washiriki 52 kutoka Kata 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ambao ni wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata na jumla ya mada kumi zitawasilishwa katika mafunzo hayo.
Wasimamizi Wasaidizi hao wamekula kiapo cha kutunza siri na kutoa tamko la kujitoa uanachama wa chama cha siasa kabla ya kuanza mafunzo.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika tarehe 29, Oktoba 2025
"KURA YAKO HAKI YAKO JITOKEZE KUPIGA KURA"
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.