- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chemba awataka wanawake watumie vyema fursa wanazozipata kwa kuwa wao ndiyo kioo katika jamii hasa katika nyadhifa za Uongozi wanazopewa katika jamii inayowazunguka.
Afisa Maendeleo ya Jamii Bi .Mwatumu Doso aliyazungumza hayo kwenye ufungaji wa Mafunzo ya Uongozi yaliyofanyika ndani ya siku mbili katika ukumbi wa Godown ,tarehe 19 mpaka 20 Juni 2018 wilayani Chemba.
Bi.Mwatumu amesema “kwa muda wa miongo kadhaa iliyopita,wanawake wametokea kuwa wenye juhudi nyingi katika masuala ya jamii zao,lakini kunakuwepo na changamoto mbalimbali zinazowakwamisha ndiyo maana Serikali pamoja na Sekta Binafsi zinajitahidi kuwashika mikono wanawake ili wapate maendeleo”
Naye Mkurugenzi wa Shirika la UFUNDIKO(Ufundi na Uhandisi Kongwa) Ndg.Saidi Panga amesema lengo la mafunzo hayo ya siku mbili ni kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi bora na kujua majukumu yao ya msingi katika Uongozi na kuweza kujua uhusiano uliopo kati ya Viongozi na Wanaongozwa.
“Uongozi usio rasmi mahali popote una umuhimu wake na Viongozi wanapotenda shughuli zao hivyo Kiongozi anawajibu wa kutambua kuwepo kwa taasisi zisizo rasmi na kufanya kila njia kuzitumia katika kufanikisha malengo yake au ya Halmashauri kwa hiyo ni wajibu wa Viongozi kutumia njia sahihi za Uongozi ”alilisisitiza Ndg.Panga.
Katika mafunzo hayo yalishirikisha vijiji kumi na mbili ambavyo ni Tandala,Kidoka,Mondo,Goima ,Kilema Balai,Lahoda,Lalta,Jangalo,Kwamtoro,Gwandi,Mrijo Chini na Makorongo ambapo katika kila kijiji kilileta wahusika wanawake watano ambapo wapo kwenye makundi matatu likiwemo kundi la kwanza wahusika watatu kutoka kamati ya maji ya kijiji ,kundi la pili ni Muuguzi wa Zahanati na Kiongozi mmoja wa kijiji.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.