- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba amewataka Wananchi wa Wilaya ya Chemba kuweka kipaumbele suala la Afya hasa kwenye kujiunga na kadi ya bima ya Afya ambayo ya kiwango cha chini(CHF).
Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Semistatus Mashimba amesema “itakuwa jambo jema kama leo hii pesa hizi za TASAF mnazopewa mtazitumia pia katika kujiunga na bima ya Afya kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamezidi kuboresha huduma za Afya ikiwemo kupunguza kiwango cha upatikanaji wa bima ya Afya ambacho kiwango cha chini ni elfu 13000/=”
Dkt.Mashimba aliyazungumza hayo alipokuwa anafanya ziara na Viongozi wa Serikali na wa Siasa katika zoezi la kugawa pesa za TASAF katika kaya maskini katika vijiji mbalimbali ikiwemo kijiji cha Igunga tarehe 21/3/2018 na kuzungumza na Wananchi wa kijiji hicho.
Naye Mratibu wa Tasaf wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndg.Simon Butondo amesema TASAF awamu ya Tatu inatekeleza programu inayoitwa “Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini” na ni mpango wa kitaifa wa kunusuru kaya Maskini unaolenga kuongeza kipato na kutoa fursa kwa kaya maskini kwa kupewa ruzuku ya fedha ili kupunguza kiwango cha umaskini.
Aidha Mpango huo unalenga kutoa miundombinu ya Afya,Elimu na Maji ili kuboresha lishe,kuwezesha kununua mahitaji ya Wanafunzi na uzinduzi rasmi wa TASAF III ,Wilaya ya Chemba ulifanywa 11/4/2014.
Hata hivyo zoezi hilo huwa linafanyika kila baada ya miezi miwili ambapo wanaangalia kigezo kikubwa ni kaya maskini na idadi ya watoto waliopo katika familia.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.