- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga amewahamasisha wananchi watakaolipwa fidia katika kijiji cha Mwambose na Bubutole tarafa ya Farkwa kutumia pesa zao vizuri kwa malengo yenye faida .
Mhe. Simon Odunga amempongeza “Rais Mhe.John Pombe Magufuli na Waziri wa Maji kwa hatua ya haraka walioifanya juu ya Chemba hususani katika hatua ya ulipaji wa fidia kwa wananchi kwani Dodoma ishakuwa jiji na imekuwa jambo la faraja kwa wilaya ya chemba kupata mradi huo wa maji”.
Aidha Mhe.Odunga ametambulisha kikosi kazi cha kulipa fidia, kilichoundwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo ambapo ulipaji wa fidia umetoka Wizara ya Maji kupitia mapato ya serikali.
Naye Mbunge wa Jimbo la Chemba Mhe.Juma Nkamiah amesema “ rai yangu kwenu kwa kuwa Serikali ipo kwa ajili ya maendeleo nimefarijika sana na pesa hizo mtakazopata, fanyeni kwa ajili ya maendeleo, wakimama hakikisheni mnashirikiana bega kwa bega na waume zenu mnapolipwa fidia ili kutoleta migogoro ya kifamilia hasa ndoa kuvunjika kwa ajili ya ufujaji wa pesa”.
Mhe.Odunga alifanya ziara hiyo Tarehe 8/10/2019, ambapo vijiji hivyo viwili Bubutole na Mwambose wananchi wake wanahamishwa kwa kulipwa fidia na wao wamependekeza kuhamia maeneo ya Sakwaleto na Manyata.
Fidia itaanza kulipwa kuanzia tarehe 15-31/10/2019 na wananchi wametakiwa kuhama eneo hilo ndani ya siku 90 baada ya kulipwa fedha zao za fidia.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.