- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga amewataka Maafisa Kilimo kuendelea kuwapa elimu Wakulima ili waache kulima kwa mazoea kwani Mafunzo ya Kilimo yanatolewa yatasaidia kuondoa njaa na kutekeleza maagizo ya Uongozi wa Awamu ya Tano ya Mhe.Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hakuna chakula cha kugawa bure kwa wasiotaka kufanya kazi.
Mhe. Simon Odunga amesema ndoto kubwa ya Serikali ni kutoa elimu kwa jamii juu ya shughuli za Kilimo ili watu wafaidike kiuchumi kwa kuuza mazao wanayozalisha na kutumia kwa chakula.
Mhe.Simon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anafungua Mafunzo ya Ujasirimali wa Kilimo na Ufugaji tarehe 27/8/2018 katika Ukumbi wa Godown chini ya Shirika la FIDA ambapo Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 27-30/8/2018 kwa kuhusisha Wakulima na Wafugaji.
“Wakulima wengi wanalima Kilimo ambacho hakiifadhi udongo,Kilimo hifadhi ni muhimu sana kwa Maafisa Kilimo kuwafundisha wananchi kilimo cha Kontua hasa wale wanaoishi sehemu za miinuko na Maafisa Mifugo mkiwa kwenye Minada msiangalie upande wa nyama tu bali muangalie uanzishaji wa Viwanda vya ngozi kwani Tanzania inavyo vichache”aliongeza kwa kusema Mhe.Odunga.
Naye Mratibu wa Shirika la Fida International Ndg.Lomayani Laizer amesema wamekuja wilaya ya Chemba kuhamasisha Wananchi kujiunga katika Vikundi ili kuona matokeo yanayotolewa na huwa wanatumia eneo la kufanyia mafunzo kama Shamba darasa ili jamii iweze kujifunza kwa kuona kuhusiana na mafunzo yanayotolewa.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.