- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WANAFUNZI ZAIDI YA 1000 WA SHULE YA MSINGI CHEMBA WANUFAIKA NA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO.
Zaidi ya Wanafunzi 1000 wa Shule ya Msingi Chemba wanatarajiwa kunufaika na huduma ya upimaji macho inayotolewa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Hospitali ya Benjamin Mkapa, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma, na timu ya Wataalam wa macho kutoka Chuo cha macho Hongkong Polyclinic
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Marko Mgonja tarehe 14, Agosto 2025 wakati zoezi la macho likiendelea shule ya msingi Chemba.
Pamoja na kuishukuru Wizara ya Afya, Hospitali ya Benjamin Mkapa, Ofisi ya Mganga Mkuu Dodoma Kwa kushirikiana katika utoaji wa huduma hiyo Dkt. Mgongonja amesema kuwa ni vizuri utaratibu wa kupima matatizo ya macho kwa watoto ukafanyika mara kwa mara nchini ili kuwabaini watoto wenye matatizo ya macho na kuwatibia wakiwa bado wadogo kwani itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.
“Kuna Watoto wana matatizo ya macho na Wazazi/Walezi hawajui kama Watoto wao wana matatizo ya macho, hali hii inawapelekea kutokufanya vizuri darasani hivyo huduma hii itawasaidia kugundua matatizo waliyonayo na kupatiwa matibabu sahii” amesema Mgonja
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa amesema kuwa mara baada ya kufanyiwa vipimo watoto wenye matatizo ya macho watatibiwa katika vituo vya huduma za afya ngazi ya Wilaya, wengine watapewa rufaa kwenda Hospitali ya Benjamini Mkapa na wenye mahitaji ya miwani watachukuliwa vipimo na baadaye kutumiwa miwani na Wataalam hao wa macho kutoka Chuo cha Hong kong Polyclinic.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.