- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amewataka waajira wapya wa Serikali kuwajibika kazini kwa kufata kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi Dkt.Semistatus Mashimba aliyazungumza hayo alipokuwa na Watumishi wapya ambao ni Maafisa Watendaji wa Vijiji wa Wilaya ya Chemba katika ukumbi wa Godown tarehe 25/6/2018.
Dkt.Semistatus Mashimba “Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutoa kibali cha ajira mpya, na mnapaswa kufanya kazi kwa bidii bila kusahau kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa kuwasikiliza na kuwatumikia Viongozi wa Serikali,Wanasiasa ,Wadau mbalimbali pamoja na Wananchi kwa ujumla”
Naye Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bi.Carolina Kayombo amesema suala la ajira walipata kibali kutoka Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora cha kuajiri Maaafisa Watendaji 33 ,ambapo mnamo tarehe 10 na 11 mwezi wa 5/2018 ambapo walifanya usaili kwa ajili ya kupata hao Watumishi na kufanya taratibu za kuwaajiri.
Bi.Carolina Kayombo aliongeza kwa kusema “bado tunaendelea kuwapa maelekezo namna ya kufata taratibu za Utumishi wa Umma hasa Muongozo wa Kiutumishi kwa sababu tunaamini wametoka sehemu mbalimbali ikiwemo vyuoni moja kwa moja na wengine wametoka vyuoni muda mrefu kwa hiyo siyo wote wanajua taratibu za Utumishi ndiyo maana tukaamua kukaa nao ili kuwapa Elimu hiyo”
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.