- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amepokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Mkoa wa Dodoma (UWT) walipowatembelea wahanga wa mafuriko ya mvua , tarehe 3/2/2018.
Mwenyekiti Dkt.Semistatus Mashimba amesema ataendelea kuwa bega kwa bega na watu waliopata maafa ya mafuriko ya mvua yaliyotokea January 2018 katika kata ya Mrijo kwa kuwatafutia misaada mbalimbali kwa ajili ya kujikimu.
“Mpaka sasa watu 174 wako kambini, tayari timu ya watalaam ya watu watano wa kupima ardhi wapo kata ya Mrijo , mbegu tani 7 za mahindi, tani 5 za mtama, zimetolewa kutoka Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Wahanga na kipaumbele ni kupatiwa waathirika wote”amesema Dkt.Mashimba.
Dkt.Mashimba amesema tayari Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilishatoa kilo 100 za sukari, lita 100 za mafuta ya kula na gunia 20 za unga wa mahindi.
“Naishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, Viongozi wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Dkt.Binilith Mahenge kwa kuwa nasi bega kwa bega na Wataalam wake kutoka mkoani, Mbunge wa Jimbo la Chemba Mh. Juma Nkamia na Wadau mbalimbali wanaotoa misaada kwa wahanga wa Mafuriko ya Mvua.” alisisitiza Dkt.Mashimba.
Naye, Mbunge wa Viti Maalam jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Felista Bura amesema walisikia taarifa ya maafa kutoka kata ya Mrijo katika vyombo vya habari na wakaamua wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Mkoa wa Dodoma kuja kutoa misaada mbalimbali kwa wahanga hao .
“wanaopata maafa asilimia kubwa ni akinamama na watoto ndiyo wanaoteseka, hivyo waathirika wote mtakaopata maeneo mapya ya viwanja yaliyopimwa kwa ajili ya kujenga nyumba ni vyema muhamie haraka ili muanze kujenga na muendelee kuishi maisha ya kawaida ya kila siku .” Alisisitiza Mh. Bura.
Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Mkoa wa Dodoma (UWT) umetoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo sabuni katoni 10, nguo, unga wa mahindi viroba 5 vya kg 25, vitenge doti 10, gunia moja la mahindi na fedha taslimu laki moja.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.