- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya Fedha na Uchumi H/w ya Chemba imefanya ukaguzi wa ujenzi wa Miundo Mbinu katika kijij cha Mondo katika utekelezajiwake wa kila mwezi ili kuhakikisha fedha zinazotolewa zinaendana nauhalisia wa matumizi yanayohitajika(value for money) katika miundo mbinu hiyo.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 23/1/2018ikihusisha Madiwani ambao ni wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Wataalam kutokaHalmashauri ya Wilaya ya Chemba.
Aidha Mkuu wa Idara ya Maji Mhandisi.Rodrick Mbepera amesema Mradi wa ujenzi wa Miundo mbinu katika kijiji cha Mondo, kata ya Mondo unaendelea vizuri kwa usimamizi wa Mkandarasi M/S IWAWA & BUILDING WORKS CO.LTD.
Mhandisi Mbepera aliongeza kwa kusema “ Benki ya Dunia imetoa kiasi cha Tsh. 673, 898, 236.00 kwa ajili ya kugharamia Mradi huo,ambapo Miundo mbinu ya ujenzi wa tenki lita 1,000,000, ujenzi wa vituo 13 vyakuchotea maji, ujenzi wa nyumba ya mtambo wa maji, ujenzi wa nyumba ya mlinzi,ujenzi wa ofisi ya jumuiya ya watumiaji maji, ujenzi wa milambo miwili, ujenziwa tenki lita 50,000 katika shule ya sekondari Mondo na uchimbaji wa mitaro naulazaji wa mabomba unatekelezwa.”
Mradi huo ulianza Agosti, 2017 na utamalizikaFebruari, 2018.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.