- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu tarehe 17, Septemba 2025 amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha kwa Watumishi wa Serikali katika Halmashauri hiyo tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Agosti, 2025 kushika Wadhifa huo.
Akizungumza na Watumishi wa Serikali Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Kazungu amewataka Watumishi hao wanapotekeleza majukumu yao kuzingatia kanuni, sharia na taratibu za utumishhi wa Umma sambamba na dira ya Taifa ya maendeleo 2050 na kuitafsiri kwa vitendo Dira hiyo ili waweze kufikia malengo ya dira hiyo.
Aidha, Dkt Kazungu amewataka Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuhakikisha kuwa Watumishi wanapata haki zao za msingi katika utumishi ikiwa ni pamoja na haki ya kupata likizo, Haki ya uhamisho, haki ya kulipwa posho na kuimarisha mahusiano mazuri kazini.
“Mkoa wetu wa Dodoma ndiyo Makao makuu ya Nchi, hivyo ni vyema Wananchi wawe na kipato cha uhakika ili kujikimu na familia zao hivyo sisi kama Viongozi ni lazima tubuni mikakati hasa katika uzalishaji” amesema Dkt. Kazungu
Sambamba na hilo Dkt Kazungu ameielekeza Ofisi ya Mkurugenzi Chemba kutenga maeneo ili Wananchi wa Chemba waweze kushiriki kikamilifu katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kuongeza kipato cha Mkoa na ajira.
Hata hivyo, Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Dodoma akatumia fursa hiyo kuwakumbusha Watumishi wa Chemba kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba, 2025
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.