- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Alphonce Chilimo,
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg. Jofrey Pima akifungua mafunzo ya uandikishaji vyeti vya watoto walioko chini ya umri wa miaka mitano katika jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chemba. Ndg Jofrey Pima alisisitiza kuwa Cheti hicho kinatolewa bila malipo katika Ofisi ya Mtendaji Kata au Vituo vya Tiba (Vinavyotoa huduma ya afya ya mama na mtoto). Ila kama Cheti amepoteza au kimeharibika itampasa mzazi au mlezi kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri na atalipia shilingi 5000/= na kupatiwa cheti kingine kwa taarifa zilezile. Lengo la mpango huu ni kuondoa kabisa idadi ya watoto walioko chini ya miaka mitano ambao hawana vyeti vya kuzaliwa. Hivyo tunawaomba wazazi, walezi na wadau wengine kuhakikisha zoezi hili linafanyika kikamilifu na tuone wilaya yetu ya Chemba inakuwa ya kwanza katika mkoa wa Dodoma katika utekelezaji wa zoezi hili la kitaifa asilimia mia kwa mia.
Zoezi hili si tu litaleta faida na tija kwa watoto , wazazi na walezi bali litaleta pia faida kwa halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla kwani Serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa itapata takwimu sahihi za watoto walioko chini ya miaka mitano na hivyo kuisaidia katika kuandaa mipango mbalimbali ya maendeleo ya taifa na ya wanachemba kwa ujumla.
Zoezi hilo la Kitaifa lilianzia mwaka 2012 hadi 2018 katika Mikoa ya Dar es Salaam (Temeke), Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa, Njombe, Shinyanga, Geita, Lindi, Mtwara, Mara na Simiyu na kwa sasa linaendelea katika Mikoa ya Dodoma na Singida kuanzia tarehe 15 Machi 2019 na kuendelea na ni zoezi la kudumu. Mpango huo umedhaminiwa na UNICEF, CANADA na TIGO kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na baadae mpango huu utaendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Kaimu Mkurugenzi pia alieleza umuhimu wa cheti cha kuzaliwa kuwa ni;
Kaimu Mkurugenzi pia aliwataka wasajili na watoa vyeti kukumbuka kuwa:
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.