- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wananchi waache tabia ya kuficha Waharifu wa kuharibu barabara kwa kutoa alama za barabarani ,kwani Serikali imetumia gharama nyingi kutengeneza barabara ya Dodoma hadi Babati,atayefanya uhalibifu wa barabara hiyo atachukuliwa hatua kali za kisheria na wakumbuke aliwaahidi toka kipindi cha Uchaguzi atakamilisha zoezi la Ujenzi huo.
Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli aliyazungumza hayo alipokuwa anazindua barabara hiyo yenye Kilomita 251 wilayani Kondoa mkoani Dodoma tarehe 27 Aprili 2018 na kuhudhuriwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dkt.Akinumwi Adesina na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe.Masaharu Yoshida .
Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli amesema “Tunadeni kubwa la kutumikia Watanzania na lazima tufanikishe zoezi hilo tuachane na matabaka kwa misingi ya itikadi ,ukabila au dini na vyama badala yake tulete maendeleo na ilani ya Uchaguzi tutazidi kuitumikia na wale ambao siyo wanaccm tutaendelea kushirikiana nao”
Kufuatia maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Semistatus Mashimba ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Rais Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuweza kukamilisha barabara ya Babati kwenda Dodoma ambapo kwa Wananchi wa Chemba wananufaika kupitia barabara hiyo katika kufanya shughuli zao za kimaendeleo.
“Wananchi wa Chemba kupitia barabara hiyo watanufaika katika kipindi cha kuuza mazao yao kwani kwa mwaka huu tunatarajia mavuno ya kutosha kutokana na wananchi wetu kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la watu wanapaswa kulima na hatagawa chakula kwa watu ambao hawajalima na badala yake walime ‘aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Mashimba
Hata hivyo kazi za ujenzi ziligawanywa katika sehemu kuu nne ambazo ni Dodoma-Mayamaya (Km43.65),Mayamaya-Mela (Km 99.35), Mela-Bonga (Km88.8),Babati-Bonga (Km16.2) na (Km3) za kuingia Kondoa Mjini na mradi huo umegharimu shilingi bilioni 378.4.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.