- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
OVADA WAPONGEZWA KWA KUCHANGIA NGUVU ZA WANANCHI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
“Nawapongeza sana kwa kuchangia nguvu zenu katika utekelezaji wa miradi ya maendendeleo katika Kata hii ya Ovada, nawaomba muendelee hivyohivyo kuunga mkono juhudi za Serikali”
Pongezi hizo zimetolewa na na Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash tarehe 20, Agosti 2025 Kata ya Ovada alipokua akihitimisha ziara zake za kutembelea kata 26 za Wilaya ya Chemba kusikiliza na kujibu kero za Wananchi.
“Taarifa yenu inaonyesha kuwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wananchi wa Kata ya Ovada mmechangia nguvu zenu kwa zaidi ya shilingi mil. 20, hongereni sana” amesema DC Okash
Aidha Mhe. Okash amewataka Wazazi/ Walezi katika Kata hiyo ya Ovada kuwapaeleka Watoto shule wakasome na kuhakikish watoto hao wanafaulu ili waweze kujisimamia vizuri katika masha yao siku zijazo.
“Dunia ya sasa inahitaji wasomi, hata ukiwarithisha mashamba kama hawana elimu watashindwa kuyasimamia vizuri mashamba hayo, nasisitiza sana kuhusu elimu kwasababu elimu ni haki ya msingi kwa kila mtoto na elimu ndiyo kila kitu” amesema Mhe. Okash
Sambamba na hilo DC Okash amekemea tabia ya unywaji pombe uliopitiliza na hasa nyakati za asubuhi na hivyo amemuelekeza OCD kuanza msako haraka wa kuwakamata wote wanaofungua vilabu vya pombe nyakati za asubuhi.
Kwa upande wake Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kwamtoro Bi Selina Lasway kwa niaba ya Wakazi wa Tarafa ya Kwamtoro amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha zaidi ya sh. Bil 2 ambazo zimetumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya afya, elimu,barabara na mikopo ya 10% kwa vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.