- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba leo Julai 9, 2025 Ndugu Hassan Mnyika wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Walimu ( Ajira mpya) wa shule za Sekondari na Shule za Msingi yaliyofanyika katika Ukumbi wa MIKUTANO WA hALMASHAURI.
Mkurugenzi Mnyika amesema kuwa Elimu ndiyo msingi wa kila kitu hivyo amewataka Walimu hao wakafanye kazi kwa bidii, wafuate taratibu za Utumishi wa Umma , waboreshe viwango vya ufaulu ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake katika sekta hiyo muhimu.
"Ukiwa Mtumishi wa Umma unatakiwa kuwa mfano bora katika Jamii kimaadili, hivyo yeyote atakayekiuka taratibu hizo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake" Amesema Mkurugenzi Mnyika
Aidha, Ndugu Mnyika amesema kuwa yeye kama Mwajiri wa Walimu hao yuko tayari kushirikiana nao bega kwa bega ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha ambapo pia amewaomba Walimu ha o watakapokutana na changamoto mbalimbali wasiume peke yao bali wawashirikishe Viongozi wao.
Mapema akizungumza na Walimu hao Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Ndugu Josephat Ambilikile amesema kuwa Walimu Waliopatiwa mafunzo elekezi ni Walimu 53 wa Shule za Sekondari na Walimu 40 wa Shule za Awali na Msingi.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.