- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelin Mabula amwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataalam wake kusimamia kikamilifu katika kutatua kero mbalimbali za ardhi ya wananchi ikiwemo kufatilia hati miliki za wananchi mahali husika, siyo paka kusubiri waletewe ofisini na kubadilika ikiwemo kubadilisha mifumo ya kizamani na kuendana na ya kisasa ambayo itawasaidia kukusanya mapato makubwa.
Dkt.Angelin Mabula aliyazungumza hayo ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba alipokuja kuhamasisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali ikiwemo kodi ya Ardhi ,Urasimishaji ,Tarehe 23/1/2019.
"Aidha tumekuja Chemba kuhamsisha ukusanyaji wa maduhuli kupitia kodi ya ardhi na mnapaswa muwe na mapato makubwa ya ukusanyaji kodi kwani nikiangalia mnayo maeneo makubwa ambayo mnapaswa kuhamasisha wananchi kwa wingi ndani na nje ya chemba kuja kununua ya makazi na uwekezaji lakini mna kiwango kidogo cha malipo ya viwanja vilivyolipiwa na acheni tabia ya kuwalea wadaiwa sugu" Mhe.Angelin.
Naye Mkurugenzii Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba amesema kwa upande wa makazi ni changamoto hata kwa wafanyakazi wa Halmashauri,kwani makazi ni machache ndiyo maana waliamua kuuza viwanja hadi kwa wafanyakazi ili iwe rahisi kuishi hapo kwa bei ya chini ambapo wengi wao walilipokea hilo.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndg.Enock Mrigo alizungumzia shughuli wanazozifanya ikiwemo ubunifu wa mipango miji ikiwemo kuendeleza mji wa Chemba na kutatua migogoro ya ardhi ndani ya wilaya na inaendelea kutatuliwa kwa ngazi ya Taifa,Mkoa,Wilaya,Kata na Vijiji na kingine kuwa na watumishi wachache nayo changamoto.
Alitolea mfano mgogoro wa mipaka , mpaka kati ya Wilaya ya Chemba (Kijiji cha Handa) na Wilaya ya Singida Vijijini (Kijiji cha Kazamoyo) ,hatua zilizochukuliwa ni Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Singida vijijini waliitisha kikao cha ujirani tarehe 26/10/2017 kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama za wilaya zote pamoja na Wataalamu wa Ardhi na Upimaji wa Halmashauri zote mbili na kuamua kuhakiki upya mpaka huo ili kuondoa utata kwa mujibu wa ramani za wizara y ardhi 2008.
Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga alimuomba Naibu Waziri Mhe.Angelin awasaidie kwenye kutatua migogoro ya mipaka kwenye hifadhi za Taifa kama Mhe.Rais John Pombe Magufuli alivyoagiza pamoja na kuomba kujengewa nyumba za watumishi kupitia shirika la nyumba NHC ili waweze kuishi na kufanya kazi kiurahisi ambapo hivyo vyote Mhe.Angelin aliahidi kuvitekeleza.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.