- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Godwin Mkanwa awataka Wenyeviti na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi kutumia nafasi zao katika kuhakikisha wanachapa kazi na kufatili kila miradi ya kimaendeleo inayoletwa na Serikali ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa hasa kwa kushirikiana vizuri na Wataalam husika wa miradi hiyo inayoletwa au kujengwa.
Godwin Mkanwa amesema "Kumekuwa na kelele nyingi hasa kwenye miradi inayojengwa ikiwemo mafundi kutolipwa kwa wakati,wataalam husika kuratibu miradi kinyume na utaratibu badala yake kuweka pesa mifukonu, kumbukeni Serikali ipo kwa ajili ya kupunguza vifo vya kinamama na watoto na kutua ndoo kichwani, sasa jambo la afya na maji ndiyo suala linalowekewa kipaumbele, mnatakiwa kuwa makini na mnapaswa kubadilika"
Aidha hata katika Chama changu sitakubali mtu yoyote anayekwamisha miradi ya kimaendeleo ya Kitaifa ni vyema kila mmoja wapo awajibike na inasikitisha wadau mbalimbali wanatoa fedha ili kuhakikisha Chemba inakuwa lakini cha kushangaza miradi mingi inasimama paka pesa zinakwisha mnashindwa kutoa taarifa mapema.
Aidha Mkanwa amesema angependa wataalam wafanye kazi zao na tambueni tupo kwa ajili ya maslahi ya wananchi,kusiwe na mwingiliano wa kisiasa ambao utasababisha marumbano na muungiliano wa kimajukumu ambao utaleta sitofahamu badala yake kufanya kazi kwa mipaka pasipo kuleta visingizio na kushirikiana ili kuijenga Chemba.
Mkanwa amefanya ziara ya Kamati ya siasa ya mkoa ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,ikiwa ni ulekezaji wa ilani ya Ccm ambapo alitembelea miradi inayojengwa ikiwemo kituo cha polisi Chemba,Kituo cha Afya Hamai,Jengo la Halmashauri ya Chemba na Hospitali ya Chemba, Tarehe 24/1/2019.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.