- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na. Alphonce Chilimo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Chemba ambapo ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti ngazi ya Wilaya iliyofanyika Januari 3 2023. Ikiwa uendelezaji wa kampeni iliyozinduliwa rasmi Desemba 31 2022 kwa kupanda miti kwenye eneo la chanzo cha maji cha DUWASA kilichopo eneo la Ihumwa vijijini.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhe. Senyamule amewataka wasimamizi wa eneo hilo, wadau wa mazingira na wananchi kulipa kipaumbele bila kusukumwa kwani kila mmoja anapaswa kutambua wajibu wake juu ya kulinda mazingira endelevu kutokana na umuhimu wake.
Ametoa msisitizo mashuleni akiwataka walimu kusimamia zoezi la upandaji miti mashuleni kwa utaratibu wa kila mwanafunzi kupanda mti mmoja na kuutunza hadi atakapomaliza shule. Ni wajibu wetu kutunza mazingira na vyanzo vya maji kwa kupanda miti kwa wingi huku tukizuia ukataji wa miti hovyo. Sitatamani kuona uzembe wowote ambao utatokea wa kuifanya miti hii isikue, Nitoe onyo kwa wananchi ambao ni chanzo cha uharibifu wa miti kuwa ni kinyume cha sheria na tutawachukulia hatua “Ameongeza Mhe. Senyamule.
Vilevile, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simoni Chacha ametilia mkazo zoezi hilo la upandaji wa miti maeneo ya ulangini kwa kuwa ndio maeneo yaliyoathiliwa sana na ukataji wa miti ukilinganisha na maeneo ya usandaweni ambapo wanakijiji hao hawana tabia ya ukataji miti hovyo. Amewataka wananchi kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri kuchukua miti na kuipanda maeneo yao angalau kila nyumba kuwa na miti angalau mitano. Takribani miti 300 ilipandwa katika eneo hilo la Hospitali na wilaya ya Chemba inatarajia kupanda miti 1,500,000.
Sanjali na zoezi la upandaji miti Mkuu wa Mkoa pia amezungumzia masuala ya uchangiaji chakula mashuleni ili watoto waweze kupata chakula angalau cha mchana waweze kupata utulivu madarasani. Pamoja na uchangiaji chakula amewataka wakuu wa wa shule kuanzisha mashamba ya shule yaliyotelekezwa mda mrefu ili wanafunzi waanze kuyalima ikiwa ni sehemu ya kupata elimu ya kujitegemea watakapomaliza shule.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.