- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewataka Wataalam wa Kilimo na Mifugo kutoa Elimu ya kutosha kwa Wakulima na Wafugaji kwa sababu chanzo cha mapato katika Wilaya ya Chemba ni Kilimo na Mifugo.
Mhe.Simon Odunga aliyazungumza hayo katika Ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa Wataalam wa Kilimo na Mifugo iliyoendeshwa na Tume ya Taifa ya Science na Tecknolojia (COSTECH) katika Shule ya Msingi Chemba ,tarehe 13/1/2018.
“Msimu huu ni wa Kilimo na nimefurahi mmekuja kipindi kizuri ambacho kitawawezesha Wataalam wetu kuwaelimisha Wakulima kuhusu Teknolojia mliyowapa kwani mvua zimeanza vizuri na kuna umuhimu wa uhamasishaji ,kwa kuwa tulianza kwa kuzindua Msimu wa Kilimo Wilaya ya Chemba ,tarehe 14/12/2017 katika kijiji cha Mwailanje , kwa kauli mbiu ‘ONDOA NJAA CHEMBA KWA KULIMA MAZAO YANAYOTUMIA MAJI KIDOGO’aliyazungumza Mhe.Odunga.
Mhe. Odunga aliongeza kwa kusema“Mafunzo mnayoyapata siku ya leo hakikisheni mnaenda kuyafanyia kazi kwa kutembelea Wakulima na Wafugaji katika maeneo yao badala ya kukaa maofisini ili kujua ni changamoto gani wanazozipata ,njia zipi mnawapatia ili kuepukana na ufugaji wa kiholela na Kilimo cha kimazoea”
Naye Mratibu wa Mradi huo Ndg,Philbert Nyinondi amesema malengo ya Mradi huo ni kueneza teknolojia bora zilizozalishwa katika vituo mbalimbali vya utafiti nchini na mafunzo hayo ni muhimu kwa maendeleo ya Kilimo katika Wilaya ya Chemba.
Pia katika mafunzo haya tumeleta mbegu za mahindi yanayoendana na hali ya hewa ya Dodoma kwa ajili ya mashamba ya majaribio yatakayotumiwa na Maafisa wa Kilimo kuelimisha Wakulima kwa njia ya Vikundi.
Mafunzo hayo yameshirikisha Mkuu wa Wilaya ya Chemba ,Wataalam wa Kilimo na Mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ,Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH), Wataalam kutoka chuo Kikuu cha Sua na Vyuo vya Utafiti.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.