- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewataka Wananchi wa Kijiji cha Kwamtoro kata ya Kwamtoro waache tabia ya kuchukua maeneo kiholela badala yake wafuate kanuni na taratibu za kumiliki ardhi kwani Serikali inapoteza rasimali fedha na muda katika kutatua migogoro ya ardhi ambayo wananchi wanafanya.
Mhe.Simon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anafanya Mkutano wa hadhara akiwa na Mkurugenzi wa H/W Chemba,Wataalam, Kamati ya Ulinzi na Usalama tarehe 20/8/2018 katika kijiji cha Kwamtoro kata ya Kwamtoro.
Mhe.Simon Odunga amesema “Wananchi wamekuwa na tabia ya kuvamia maeneo na hata wakipewa maeneo kihalali wanatabia ya kuyauza maeneo hayo na kukimbilia kuvamia maeneo ya umma kitendo ambacho siyo kizuri, kinababisha serikali kupoteza muda kuendelea kufuatilia nini kifanyike na wengine wanajua kabisa maeneo wanayoyachukua au kukaa ni kwa ajili ya shule, masoko na stendi za mabusi”.
Aidha amewataka wakazi wa kijiji cha Kwamtoro waliojenga nje ya utaratibu katika maeneo ya soko, stendi na shule watoke haraka sana ndani ya siku 90 na baada ya muda huo kupita watatolewa na serikali.
Pia, amewataka Viongozi wa siasa na Serikali wa vijiji na kata Wilayani Chemba wasipende kutoka nje ya taratibu na kusababisha uchochezi bali wawaelekeze wananchi wafuate taratibu za kumiliki ardhi ili kutekeleza maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H. Mashimba amesema Serikali haiwezi kuwaonea wananchi wake, kwani ni sawasawa na baba kumuonea mwanae ,badala yake wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu wanao wauzia maeneo ambayo siyo yao bali yanamilikiwa na umma .
Dkt.Mashimba aliongeza kwa kusema “kwa wale wenye tabia ya kujenga maeneo ambayo siyo yao na kutegemea fidia wakati wa kuondolewa na Serikali waache tabia hiyo mara moja kwani mambo ya kupeleka kesi mahakamani wakati wanajua wapo kinyume na taratibu wanaisababishia Serikali kutumia gharama kubwa kuendesha kesi mahakamani na kupoteza muda”.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.