- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amezindua kampeni ya kisiki kilicho hai ikiwa na lengo la kutunza mazingira kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali liitwalo Lead Foundation.
Mhe.Simon Odunga amesema utunzaji wa mazingira na lishe unamahusiano makubwa ni vyema wakaachana na tabia ya uchomaji miti ovyo kwani juhudi zinaendelea ikiwemo Wakala wa Misitu nao wameweka Sheria kali juu ya hilo.
‘’Mkumbuke Chemba inashida ya maji,mkombozi wetu ni miti ikiwemo Kisiki hai ambacho hakihitaji maji bali kukombolewa na kitatusaidia kwenye maji,acheni tabia ya Wakulima kufyeka sehemu yote ya shamba badala yake muwe munaacha miti pembezoni mwa mashamba ambapo inasaidia kulinda mipaka ya mashamba”
Lead Foundation iliandaa programu ya miaka mitatu inayolenga kuwezesha kaya 200,000 katika vijiji 300 vya mkoa wa Dodoma,kutumia njia ya kisiki hai ifikapo 2021 lengo ni kueneza njia hii Mkoa wote wa Dodoma na nchi nzima kwa kustawisha miti ili kutunza uoto wa asili.
Uzinduzi huo ulizinduliwa Tarehe 19/10/2018 na kushirikisha baadhi ya wadau kutoka katika vikundi mbalimbali vya mazingira vilivyopo Chemba, Watumishi wa Halmashauri na Waheshimiwa madiwani katika ukumbi wa godown Chemba.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.