- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba akutana na Asasi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii na kuzungumza na Watafiti hao walioelekezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kuandaa mazingira ya uwekezaji Mkoa wa Dodoma.
Dkt.Semistatus Mashimba amesema “Dodoma ni Makao Makuu ya nchi na muhimu ijipambanue tofauti na miji mingine,na ni vizuri katika uwekezaji wakaangalia maeneo husika kwa kuzingatia nguvu kazi na gharama husika ya fursa zilizopo”.
Dkt.Semistatus Mashimba aliyazungumza hayo alipokutana na Watafiti hao wa Kiuchumi na Kijamii(Economic and Social Research Foundation-ESRF) na Menejiment a ya Halmashuri ya wilaya ya Chemba, Tarehe 11/9/2018.
Aidha pia Dkt.Mashimba alitoa ushauri Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara kuwa na muundo wa pamoja au kuunda wakala utakaosimamia uwekezaji ,hususani katika viwanda.
Katika majadiliano hayo watafiti walipokea mapendekezo hayo na kuahidi kuyawasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.