- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba ameitaka Kamati ya Ujenzi katika ngazi ya kijiji kusimamia kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa Zahanati kwa kuhamasisha jamii kuchangia nguvu kazi na kuitaka Kamati izingatie uadilifu ,uaminifu katika kutekeleza zoezi hilo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa Mjumbe yoyote atakayekwenda kinyume na sheria.
Dkt.Semistatus Mashimba aliyazungumza hayo kwenye Mkutano wa hadhara wa kuhimiza Wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo na alisisitiza Wananchi kushiriki kwa karibu kwenye Uboreshaji wa Miundo Mbinu ya Kituo cha Afya katika kijiji cha Hamai kata ya Songolo tarehe 24/1/2018.
Dkt.Mashimba amesema “Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli imeikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Tsh.milioni 400 kwa ajili ya maboresho ya kituo cha Afya Hamai, na tayari fedha hizo zipo kwenye akaunti ya H/W ya Chemba kwa ajili ya kukabidhi kwenye akaunti ya kijiji cha Hamai .”
“Maboresho ya Ujenzi unaanza mara moja kuanzia tarehe 24/1/2018 chini ya Kamati ya Ujenzi na Wananchi wakumbuke Kituo hiki cha Afya ni kwa ajili ya kata ya Songolo, vijiji jirani ili kuepukana na changamoto ya kukosekana kwa huduma ya afya.”
Aliongeza kwa kusisitiza Dkt.Mashimba “Kwa upande wa changamoto ya upatikanaji wa maji katika kituo cha Afya ,Halmashauri ya Wilaya ya Chemba imetekeleza kwa kuchimba Kisima cha maji na mradi huo utasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji.”
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chemba Dkt.Olden Ngassa amesema mbali na fedha hizo Tsh.milioni 400 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya tano ,kuna fedha za ruzuku za maendeleo zilizotolewa kwa ajili ya kutengeneza magari ya kubeba Wagonjwa katika kituo cha Afya cha Hamai na Mrijo na mchakato unaanza mapema ndani ya mwezi Januari na Februari 2018.
Ziara hiyo ya siku moja katika kijiji cha Hamai iliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba pamoja na Wataalam ambao ni Mwanasheria, Mganga Mkuu ,Afisa Mazingira ,Afisa Manunuzi na Mwasibu.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.