- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H. Mashimba amewataka wananchi wachukue tahadhari mapema kipindi cha msimu wa mvua kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa imetabiri kutakuwa na mvua kubwa ikiwemo Mkoa wa Dodoma , ni vyema kuhama sehemu za mabondeni ili kuepukana na mafuriko.
Aidha Dkt. Mashimba amewataka Wakulima walioacha mazao yao shambani wakayavune na kuhifadhi sehemu salama.
Kwa upande wa Maafisa Kilimo,Mkurugenzi Dkt.Mashimba amewaasa kuwafundisha njia bora za kilimo ikiwemo kilimo cha kontua ili kuepukana na athari za mvua kubwa.
“Tafadhali Wananchi waliopata mavuno mnatakiwa kuyahifadhi vizuri, kuyatunza, kuachana na biashara ya kuyauza kupita kiasi mpaka akiba ikaisha ,pia acheni tabia ya kutumia nafaka yote kwenye kutengeneza pombe za kienyeji badala yake hifadhini chakula kitasaidia iwapo mafuriko yatatokea”aliongeza kwa kusema hayo Dkt.Mashimba.
Dkt.Mashimba amesema kwa upande wa Halmashauri yake ameamua kuendelea na njia bora ya kuwatembelea wananchi katika ngazi ya vijiji, kata na Wataalam wake ili jamii wazitambue shughuli wanazozifanya pamoja na kutatua kero za wananchi.
Dkt.Mashimba alifanya ziara hiyo na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kutembelea Zahanati ya kijiji cha Mapango lengo ni kufanya maadhimisho kwa ajili urekebishaji na ukamilishaji wa zahanati hiyo.
Pia walitembelea kijiji cha Chandama kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa wodi ya mama na mtoto.
Ziara hiyo ilifanyika tarehe 21 Oktoba, 2018.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.