- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba azindua UMISSETA (UMOJA WA MICHEZO SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA ) ngazi ya wilaya.
Katika uzinduzi huo, Dkt. Mashimba alijionea wanafunzi wakionesha vipaji vyao katika michezo mbalimbali ikiwemo riadha, mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa wavu, kwa kushindanishwa katika kanda nne zilizoundwa za magharibi, mashariki, kaskazini na kati.
Dkt. Mashimba alisema, “wanafunzi mnatakiwa kuonesha vipaji vyenu katika kushiriki mikchezo mbalimbali kwani Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli inathamini michezo na ndiyo maana Mhe. Rais aliunda Wizara ya Michezo, sanaa na Utamaduni kwa lengo la kusimamia na kuendeleza michezo hapa nchini”.
Wilaya ya Chemba imefanya UMMISETA kwa Lengo la kuwashindanisha wanafunzi katika michezo mbalimbali ili kuunda timu ya wilaya ambayo itaenda kushindana na Halmashauri za Wilaya ya Chamwino, Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Kondoa Mji, Kondoa Vijijini, Manispaa ya Dodoma na kuunda timu ya mkoa wa Dodoma itakayoshiriki michezo ya UMMISETA kitaifa.
Mashindayo hayo ya michezo yalifanyika tarehe 27-28 /5/2019 katika viwanja vya shule ya msingi chemba.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.