- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na, Shani Amanzi.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewapongeza wazazi na walezi wa wilaya ya Chemba kwa kuonyesha ushirikiano wa kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika Mafunzo ya Jeshi la Akiba ya Nchi yetu. “Jamii inapaswa itambue kuwa kazi ya Mgambo ni ya mtu yoyote awe wa hali ya chini au juu anaweza kupata Mafunzo lengo ni kujenga utimamu wa mwili,uzalendo na kutumikia nchi yetu hasa kwenye ulinzi na usalama wa Taifa “aliongeza kwa kusema Mhe.Simon Odunga”.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba amefurahishwa kwa ushiriki wa vijana kwenye Mafunzo hayo, hii inaonyesha dhahiri wilaya ya Chemba inaenda mbele kimaendeleo na ameahidi wanafunzi waliohitimu mafunzo atafanya nao kazi kwa ushirikiano zaidi.
Naye kiongozi wa Mafunzo hayo Meja wa Wilaya ya Chemba Joseph Narsis amesema, walianza na wanafunzi 72 na waliohitimu ni 52 kati yao wanawake 9 na wanaume 43. Mafunzo hayo yalianza Julai mosi, 2019 na kumalizika Novemba 23, 2019 changamoto ilikuwa ni baadhi ya vijana kutokuona umuhimu wa mafunzo hayo na kukatishana tamaa lakini hawa waliweza kukabiliana nazo na leo wamehitimu Mafunzo yao.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.