- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WANANCHI WA WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO
Na Shani Amanzi,
Wananchi wa Wilaya ya Chemba wamehamasishwa kutumia fursa ya mifugo waliyonayo katika kuwapatia kipato na siyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pekee kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na wingi wa mahitaji ya kifedha kwa ajili ya shughuli zao za kimaendeleo.
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi aliyazungumza hayo mapema leo 04/01/2018 alipokuwa ofisini kwake Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na kusema changamoto waliyokuwa nayo ni upungufu wa rasilimali watu na upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo(Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k )
Bw. Simon aliongeza kwa kusema “kumekuwepo na mwitikio mdogo wa Wafugaji katika uchanjaji wa Mifugo yao hasa Mbwa (kichaa cha Mbwa) na Kuku dhidi ya Kideri ,Ukosefu wa Malisho na Maji katika maeneo mbalimbali”.
“Lakini katika maboresho ya mikakati endelevu ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa Wananchi tumepiga hatua kwa kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama Kichaa cha Mbwa (Rabies) na Kideri kwa Kuku (Newscastle desease) kwa kuwachanja ili kupunguza vifo toka 20% mpaka 10% , kutibu Mifugo na kutoa tiba kwa Mifugo dhidi ya Magonjwa mbalimbali kama FMD, Minyoo na Magonjwa ya Ngozi”.
Kumekuwepo na migogoro baina ya Wakulima na Wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi hasa maeneo ya malisho na kilimo. Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Mifugo,Viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na wananchi, imekuwa katika kufanya maamuzi ya pamoja katika kutenga maeneo ya malisho ili kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.
Wito kwa wafugaji wa Wilaya ya Chemba ni kuhakikisha wanajitokeza kupiga chapa kwa maendeleo ya sekta na pia wanafuga mifugo michache yenye tija na inayoendana na rasilimali zilizopo.
Zoezi la Upigaji Chapa ni endelevu na tayari kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tumefanya zoezi kwa zaidi ya 103% ya lengo, kuelimisha wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika vijiji vya Mondo ,Hamai na Songolo ili kuongeza kipato chao na kuboresha lishe zao huku mbinu shirikishi (PPP) ikitumika kati ya Halmashauri na Kanisa la KKKT- Arusha kwenye mradi wa Mbuzi wa Maziwa.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.