- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maboresho ya Ujenzi wa Mnada wa Kijiji cha Magambua kwa ufadhili wa LOCAL INVESTMENT CLIMATE (LIC).
Na Shani Amanzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa H/W Chemba Dkt.Semistatus Mashimba pamoja na Wataalam wake wamefanya Mkutano wa hadhara, tarehe 19/8/2018 katika kijiji cha Magambua kata ya Lalta kuhamasisha ukarabati wa maboresho ya mnada wa magambua.
Dkt.Mashimba amewaeleza Wananchi kuwa tayari Halmashauri ya Wilaya ya Chemba imepokea Tsh. milioni 23 za awali kutoka (LIC) kati ya Tsh.milioni 54 ambazo katika mkataba wa makubaliano wanatoa.
Pia Dkt. Mashimba amewataka Wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa maboresho ya Mnada na wakumbuke endapo Mnada huo ukiboreshwa kutakuwa na faida kubwa kwa jamii hiyo kuuza mifugo yao.
Kwa upande wao wananchi waliridhia kushiriki katika maboresho ya ujenzi wa mnada wao na walitoa eneo ili ujenzi uanze haraka.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.