- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
"Natumia nafasi hii kuwahimiza kuwa ubandikaji wa mabango, matangazo, orodha ya majina ni kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia uchaguzi, hivyo ni wajibu wenu kuhakikisha kuwa mabango, matangazo, orodha ya majina na vyote vinavyotakiwa kubandikwa kulingana na kalenda ya utekekezaji wa majukumu ya uchaguzi unafanyika ili kuepuka malalamiko ya ukiukwaji wa masharti ya sheria na kanuni za uchaguzi"
Kauli hiyo imetolewa na Ndugu Dominick Ruhamuya ambaye ni msimamizi wa uchaguzi Jimbo La Chemba Leo tarehe 6, Agosti 2025 wakati akifunga mafunzo ya Siku tatu kwa Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata ambayo yalifunguliwa tarehe 4, Agosti 2025 ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuekekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2025.
"Tarehe 4, Agosti kabla ya kuanza mafunzo mlikula kiapo cha kutunza siri, kiapo hiki kipo kwa mujibu wa kanuni ya 8 ya kanuni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2025, hivyo ukiukwaji wa kiapo hiki uatakua unatenda kosa chini ya sheria na utawajibika kwa kosa hilo" Amesema Ruhamuya
Aidha, Ndugu Ruhamuya amewaasa Wasimamizi Wasaidizi hao kusimamia mafunzo waliyofundishwa kwa kuzingatia Katiba, Sheria na kanuni, Kutoa mafunzo kwa Watendaji wa vituo vya kupiga kura kwa weledi, kusimamia rasilimali vifaa watakavyopewa katika utekekezaji wa kazi za uchaguzi, na kuhakiki vifaa vya uchaguzi Mara tu wanapovipokea na kutoa taarifa haraka kwa msimamizi wa uchaguzi iwapo kuna mapungufu.
" KURA YAKO HAKI YAKO JITOKEZE KUPIGA KURA"
@tumeyauchaguzi_tanzania
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.