- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Ndg, Godwin Mkama amewataka Wanachama wa CCM waache tabia ya muingiliano wa kimaslahi badala yake wachape kazi kwani Chama cha Mapinduzi kipo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kimaendeleo na kudumisha amani ya Nchi.
Ndg, Godwin Mkama amesema Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli inataka Wananchi wake wa ngazi zote wafaidike na huduma za kijamii zinazotolewa na Serikali, ndiyo maana kunakuwa na ubunifu wa kubana matumizi kwa mfano ujenzi wa vituo vya afya na shule kwa kutumia mafundi waliopo maeneo husika (Force Acount) bila kutumia wakandarasi na ni vema Waheshimiwa Madiwani mkasimamia ipasavyo fedha hizo.
Mkama aliyazungumza hayo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Chemba na wanachama wa CCM, tarehe 1/9/2018 katika Ukumbi wa Godown ambapo alikuwa mgeni rasmi.
‘’Nawapongeza kwa kuanza kujenga ofisi ya chama, chama kuwa na ushirikiano mzuri baina ya Mhe. Mkuu wa Wilaya, Mhe. Mwenyeki wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji, Mhe. Mbunge, Wataalam, na mnafanya vizuri sana kuhakikisha mnatatua kero za Wananchi”aliongeza kwa kusema hivyo Ndg.Mkama.
Wakati huo huo Mhe. Mwenyekiti wa CCM mkoa aliwapokea wanachama wapya sita waliotoka vyama vya upinzani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wanachama hao ni Abdallah Ally Suti (aliyekuwa Mwenyeki wa Chama cha CUF Wilaya ya Chemba), Msongoli Yahaya (aliyekuwa Mkurugenzi wa fedha wa Chama cha CUF Wilaya ya Chemba), Salim Juma Idonga ( aliyekuwa katibu kata wa Chama Cha Chadema kata ya Kidoka), Hussein Saidi Maimbi ( aliyekuwa katibu wa tawi wa Chama Cha CUF, tawi la kijiji cha Olboloti), Abasi Nkundulo (aliyekuwa katibu wa tawi wa Chama cha CUF, tawi la kijiji cha Mwaikisabe), William Suki (aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF kijiji cha Muungano).
Aidha Mbunge wa Jimbo la Chemba Mhe.Juma Nkamia amesema Chemba ina tatizo kubwa la maji na amewaomba Wataalam wa Halmashauri wa Idara ya maji waendelee kupambana ili kuhakikisha wananchi wanapata maji maeneo yote na ameahidi kuchangia ujenzi wa Jengo la CCM Wilaya ya Chemba.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amesema Wilaya ya Chemba inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ‘’kukarabati majosho matatu katika vijiji vya Paranga, Rofati na Kidoka kwa Tshs. 1,316,000/=, pia msimu wa kilimo 2017/2018 uzalishaji wa chakula ulikuwa tani 106,652.4 na mazao ya kimkakati katika kuongezea wananchi kipato ni Alizeti, pamba na korosho.”
Mhe.Odunga amesema mafanikio hayo ya kiuchumi na kijamii inafanya Chama cha Mapinduzi kuendelea kuaminika kwa wananchi na CCM itaendelea kusimamia utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya kiuchumi na kutoa huduma za kijamii kwa ukaribu zaidi.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.