- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KIKAO CHA KATIBU TAWALA MKOA NA WATUMISHI.
Katibu Tawala Mkoa (RAS) Ndugu KASPAR K. MMUYA akishiriki kikao kazi na Watumishi wote wa Halmashauri.
Katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 29/04/2024 katika ukumbi wa Halmashauri Ndg. Kaspar alisisitiza mambo yafuatayo kwa watumishi.
UKUSANYAJI WA MAPATO
Katika suala zima la ukusanyaji wa mapato Ndg. Kaspar alisisitiwa watendaji na wakusanya mapato wengine kuifanya kazi hiyo kwa weledi huku wakitambua fika kuwa kazi waifanyayo ni ya Mhe. Rais Dr. SAMIA SULUHU HASSAN. Ndg. Kaspar aliwaomba watendaji kuto kuzima POS za kukusanyia mapato. Lakini pia alisisitiza wakusanya mapato kutokula hela mbichi na badala yake wakaziweke kwanza fedha hizo benki ndipo mchakato wa kuziomba kwa matumizi uanzishwe.
UWAJIBIKAJI.
Katika suala zima la uwajibikaji Ndg. Kaspar aliwasisitiza watumishi wote kuwajibika ipasavyo kwa wananchi kwa kauli mbiu ya “KERO YAKO NDIO WAJIBU WANGU”. Hapa aliwaomba pia watendaji wasiwe chanzo cha migogoro wanapotatua changamoto za wananchi wao kwa kuwatoza fedha ndipo watatue migogoro.
KUSIMAMIA MIRADI.
Katika swala zima la kusimamia miradi Ndg. Kaspar aliwataka watumishi wote kushirikiana hata kama mradi haupo katika Idara yako. Aidha kabla ya kikao alitembelea baadhi ya miradi ukiwamo ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Rofati kilichopo kata ya Gwandi, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi ambapo alifurahishwa na maendeleo yake.
ELIMU.
Katika swala zima la elimu Ndg. Kaspar alisisitiza ufuatiliaji kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule kuandikishwa, msisitizo pia ulitolewa katika kupunguza wanafunzi kutokuacha masomo (drop out) pamoja na ushirikiano wa wanafunzi wazazi na walimu katika kukuza ufaulu.
MENGINEYO.
Katika eneo la mengineyo lilizungumziwa swala la madeni ya watumishi waliohama kutoka Kondoa DC kuja Chemba DC. Hapa Ndg. Kaspar aliwaomba Watumishi kuwa na subira ili aweze kulifuatilia kwakuwa ni la mda mrefu sasa watumishi wa Chemba hawajalipwa wakati wilaya zingine wanalipwa.
UTOAJI WA ZAWADI KWA WATUMISHI WANAOJITOA KINAGAUBAGA.
Pia Ndg. Kaspar alishiriki zoezi la kugawa zawadi ya fedha taslimu Tshs. 500,000/= kwa watumishi wanaojitoa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki na kwa wakati. Baadhi ya watumishi
Mashuhuli ni pamoja na Mganga kutoka katika zahanati ya Mpendo aliyefanikisha zoezi la uvushaji wa chanjo katika mto bubu uliokuwa umejaa maji kitu ambacho kilikuwa ni hatari kulingana na mvua za mwaka huu.
MAELEKEZO.
Mwisho wa kufunga kikao hicho Ndg. Kaspar alitoa maelekezo kuhusu uvaaji wa utambulisho wa mtoa huduma. Alisisitiza Uongozi ufuatilie utengenezaji wa utambulisho wa mtoa huduma ili wananchi wanapotafuta huduma waweze kutambua ni nani aliyewahudumia.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.