- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mhe. Mweshimiwa Rajabu amewataka Wataalam wa Halmashauri kuendelea kuwa wabunifu na kuchapa kazi kwa bidii ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za kijamii ili Wilaya iendelee kukua.
Mhe.Rajabu aliyazungumza hayo alipokuwa kweye Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 31/8/2018 katika ukumbi wa Godown.
Mhe.Rajabu amesema “mtambue ndugu wajumbe, Wilaya ya Chemba inazidi kukua na tunaendelea kupata wageni mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo, shughuli za kiuchumi na kijamii zinatakiwa kuboreshwa ili kipato kwa wananchi wa Chemba kikue”.
Naye Katibu wa Baraza la Madiwani Dkt.Semistatus Mashimba amesema Wilaya ya Chemba bado inakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuwa na watendaji wachache wa kuajiriwa ambao wanakusanya mapato na ni vema wakashirikiana ili waweze kufanikiwa.
Dkt. Mashimba aliongeza kwa kusema “Halmashauri imepima viwanja mia nne ( 400) kwa ajili ya makazi, biashara, uwekezaji, taasisi ”, hivyo wananchi mnaombwa kuchukua fomu za viwanja kwa Tsh.20,000/= kuanzia tarehe 03/09/2018 katika ofisi za ardhi Wilaya.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.