- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ya Chemba chafanyika
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewataka wawekezaji kuja Chemba kwa wingi kwani Dodoma imekuwa Makao Makuu ya Serikali na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anaitaka Dodoma kuwa ya mfano hadi kwenye mipaka yake ya wilaya zake zizidi kuboresha miundo mbinu.
Mhe.Simon Odunga amesema moja ya changamoto zinazokwamisha wadau mbalimbali kupata nyaraka za umiliki wa ardhi (Hati Miliki) kwa wakati ni changamoto zilizopo kwenye ofisi ya Kamishina wa Ardhi na Msajili wa hati kutotoa hati miliki za Ardhi kwa wakati jambo ambalo linakatisha tamaa wadau na wafanyabiashara wa Wilaya ya Chemba.
Mhe.Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa kwenye kikao cha Baraza la Biashara kilichofanyika tarehe 8/9/2018 kwa kushirikisha wajumbe wa baraza la biashara,wataalam kutoka ofisi ya Halmashauri na afisa kutoka Local Investment Climate (LIC).
“Vyema eneo la barabara TARURA watengeneze barabara,TANESCO wapeleke nguzo na idara maji wakichimbua barabara washirikiane kwa pamoja kwenye miundombinu na idara ya mipango miji ili kuleta picha nzuri ya wilaya ya chemba iwe ya mfano kwa kujengeka kisasa”aliongeza kwa kusema hivyo Mhe.Odunga
Mratibu wa LIC-Dodoma Ndg.Donald Liija amesema katika wilaya ya Chemba wameona kuna Kituo kidogo cha Polisi lakini Ofisi ya LIC imewezesha kiasi cha Tshs.55 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikubwa cha Polisi cha wilaya ambapo ujenzi wake umeshaanza katika makao makuu ya Wilaya ya Chemba.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.