- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KIKAO CHA PAMOJA KATI YA BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA WILAYA NA WAJUMBE WA BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA YA CHEMBA KIMEFANYIKA TAREHE 16/12/2017
Na Shani Amanzi,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amewataka Wajumbe wa Baraza la Madiwani kutambua kuwa shughuli kubwa ya Baraza la Biashara ni namna gani wataangalia fursa ambazo zitatumika kwenye ngazi ya Wilaya ,Mkoa mpaka Kitaifa hasa fursa za Kibiashara na Kiuchumi na kuhakikisha zinaendelea vizuri.
Mkurugenzi aliyasema hayo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Wilaya ,ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga ,kwenye kikao cha pamoja kati Wajumbe wa Baraza la Biashara na Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Chemba kilicho fanyika katika ukumbi wa Godown wilayani Chemba ,tarehe 16/12/2017.
“Katika kikao hiki cha Baraza la Biashara na Baraza la Madiwani Wilayani Chemba ilipendekezwa kuwa ,kila Kikao cha Baraza la Biashara kuwepo na Wajumbe watatu waalikwa kutoka Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ambao ni Wenyeviti wa Kamati tatu za kudumu ambao ni M/kiti Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ,Kamati ya Afya ,Elimu na Maji,Kamati ya Ujenzi ,Uchumi na Mazingira’’alizungumza Dkt.Mashimba.
Pia Mwenyekiti wa TCCIA na Mjumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Chemba Bi.Saida Gamu amesema Diwani yoyote anaruhusiwa kutoa mchango wa kimawazo ikiwa ni lengo la kukuza biashara na uwekezaji kupitia Baraza la Madiwani au Baraza la Biashara kwa hiyo ushiriki wake katika vikao husika ni muhimu kuhudhuria ili kurahisha kutoa wazo lake la kimaendeleo kwa Wadau.
Naye Mratibu wa Baraza la Biashara Mkoa Bw.Joseph Nyalomba amesema Baraza la Biashara lilianzishwa kwa waraka namba 39 na kuzinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Mhe.Benjamin Mkapa mwaka 2001 ikiwa na lengo la kuwakutanisha Sekta Binafsi na ya Umma .
“ Ni njia bora vyombo hivi viwili vitakavyofanya kazi kwa pamoja na kutekeleza agizo la Mwenyekiti wa ngazi ya Taifa ambaye ni Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli la kuendesha Mabaraza ya Biashara ya Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kuibua fursa za uwekezaji ili kutekeleza agizo la Tanzania ya Viwanda”alisisitiza Bw.Nyalomba”.
Baraza la Biashara la Wilaya ya Chemba lilianzishwa rasmi tarehe 11/2/2016 na mnamo tarehe 3/7/2017 aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Jordan Rugimbana aliagiza kuvunjwa kwa Mabaraza yote ya Biashara ya Wilaya na kuanzishwa upya.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.